Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 Agosti 2021

12 Agosti 2021

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya vijana duniani, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuimarisha mifumo ya chakula duniani kwa kuzingatia kuwa miaka 30 ijayo watu bilioni 2 zaidi wataongezeka duniani na kuongeza mahitaji ikiwemo ya chakula.

Nchini Zambia wanufaika wa mradi wa kuimarisha lishe au SUN ulioanza mwaka 2014 wamepaza sauti zao wakielezea jinsi watoto wao wameimarika kiafya na wakati huo huo kipato cha familia kuongezeka.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, limeangazia ubunifu wenye manufaa uliofanywa na kampuni ya kuchakata mazao ya wakulima katika Visiwa vya Solomoni ambapo kampuni hiyo imebudi

teknolojia ya tanuri dogo linalohamishika na kutumia moto kukaushia mazao hasa yale ambayo yanaharibika haraka au kupungua thamani yasipochakatwa mapema.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'11"