Umoja wa Mataifa unaendelea kuwapatia msaada wananchi waliosalia nchini Ukraine
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu.
Wakazi wa Chasiv Yar mkoani Donetsk tangu kuibuka kwa vita kati ya Ukraine na Urusi wamekuwa wakiishi katika hali ya taabu na kujificha katika mahandaki chini ya nyumba zao.