Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© FAO/Aamir Qureshi

Pamba ni zaidi ya kitambaa cha nguo

Leo ni siku yap amba duniani ikiwa ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku hiyo kuenzi zao ambalo kitabaa chake kinatengeneza mavazi ya kila siku kwenye mkabati mengi ya nguo ni kitambaa kizuri, rahisi kuvaa, kukitunza na kinadyumu kwa muda mrefu. Lakini kwa mujibu wa Umoija wa Mataifa pamba inawakilisha zaidi ya kitambaa kama inavyofafanua taarifa ya Flora Nducha 

Sauti
2'40"
© UNICEF/Andrew Esiebo

WHO yaridhia chanjo ya Malaria kwa watoto

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus akitangaza pendekezo la WHO la "matumizi mapana ya chanjo ya kwanza ya malaria ulimwenguni," amesema kuwa chanjo iliyosubiriwa kwa muda mrefu "ni mafanikio ya sayansi, afya ya mtoto na malaria." Taarifa ya Jason Nyakundi inaeleza zaidi. 

Sauti
2'52"
PAHO/WHO/Karen González Abril

Umaskini wa kupindukia katika kila hali wakumba zaidi watu wa makabila, makundi na rangi fulani pekee

Watu bilioni 1.3 katika nchi 109 duniani ni maskini wa kila hali na kiwango cha umaskini huo kinatofautiana kikabila, kwa kundi au rangi, hiyo ni kwa mujibu wa uchambuzi mpya kuhusu kiwango cha umaskini wa kila hali duniani ikiwemo kiafya, kielimu na kiwango cha maisha, uliotolewa leo na Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Taarifa ya Anold Kayanda inafafanua zaidi.

Sauti
2'26"
UN Tanzania

FISH4ACP kunasua wavuvi na wachuuzi wa samaki Katavi nchini Tanzania

Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limetambulisha mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika mkoani Katavi baada ya mradi huo unaohusisha nchi 12 za Afrika, Karibea na Pasifiki kuwa na matokeo chanya kwa wavuvi mkoani Kigoma. Devotha Songorwa wa Radio washirika KidsTime FM anafafanua zaidi katika ripoti hii.

Sauti
4'27"
© WFP

Hali ya watoto kiafya nchini Afghanistan ni muhali, unyafuzi umekithiri- UNICEF

Hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula na vita nchini Afghanistan vimeongeza mara dufu tatizo la utapiamlo kwa watoto na kuzusha wasiwasi mkubwa kwa hatama ya watoto hao na familia zao yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP ambayo sasa yametoa wito wa mshikamano kunusurua taifa hilo. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Sauti
2'26"
UNMAS

Mabomu yateguliwa huko Sudan Kusini, raia wafurahia

Nchini Sudan Kusini wakati sasa milio ya risasi inaweza kuwa imepungua katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, jinamizi la vita vya wenyewe kwa wenyewe bado linawaandama hasa kwa kuzagaa kwa manbaki ya silaha za vita kama mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya mlipuko, ambavyo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayochukua hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS ni tishio la kila siku kwa maisha ya wanawake, watoto na wanaume kwenye maeneo mbali mbali nchini humo . Flora Nducha anaelezea zaidi. 

Sauti
2'11"
© UNICEF/Juan Haro

Mwalimu kushiriki kwenye mipango ya kuwainua walimu ni jawabu la sekta ya ualimu duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na wadau wake linasema ufufuaji wa elimu unaofanikiwa unategemea kuongezeka kwa uwekezaji katika ustawi, mafunzo, ukuzaji wa kitaalam na hali ya ufanyaji kazi ya waalimu milioni 71 ulimwenguni ili kurejea katika hali nzuri baada ya kupotea kwa muda wa masomo kutokana na Covid-19. Taarifa ya Lucy Igogo ina maelezo zaidi.  

Sauti
2'44"
IOM/Kaye Viray

COVID-19 yaacha kiwewe miongoni mwa watoto na vijana

Watoto na vijana watasalia na madhara ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 kwa afya zao za akili na kimwili kwa miaka mingi ijayo, imesema ripoti mpya ya hali ya watoto duniain ilyotolewa leo jijini New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni, UNICEF. Maelezo zaidi anayo John Kibego.
Hamjambo? Sote tunapata msongo wakati huu wa COVID-19!!

Sauti
2'42"