Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 yaacha kiwewe miongoni mwa watoto na vijana

COVID-19 yaacha kiwewe miongoni mwa watoto na vijana

Pakua

Watoto na vijana watasalia na madhara ya ugonjwa wa Corona au coronavirus">COVID-19 kwa afya zao za akili na kimwili kwa miaka mingi ijayo, imesema ripoti mpya ya hali ya watoto duniain ilyotolewa leo jijini New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni, UNICEF. Maelezo zaidi anayo John Kibego.
Hamjambo? Sote tunapata msongo wakati huu wa COVID-19!!
Ndivyo asemavyo mtoto Lova Annah, maarufu katika mitandao ya kijamii nchini Madagascar akisalimu na kisha anaelezea mambo matano muhimu aliyofanya wakati wa vizuizi vya janga la COVID-19 ili kulinda afya ya akili.
Tulicheza karata! Tulichora! Tulikula vitamutamu na mama jikoni na watoto wengine,  Lova anasema cheza karata, chora picha, tuliimba na Romeo na pia jioni tulitazama televisheni na baba na mama na watoto wengine!
Mbinu kama za Lova zilihitajika kwa kuwa ripoti ya UNICEF ikipatiwa jina Katika Fikra Zangu: Kuendeleza,kulinda na kuhudumia afya ya akili ya watoto, inasema hata kabla ya Corona watoto na vijana walibeba mzigo wa afya ya akili katika jamii ambazo hazina uwekezaji wa kutosha katika afya hiyo.
Ripoti hiyo ikijikita kwa kina katika afya ya akili kwa watoto, vijana na walezi katika karne ya 21 imesema hata kabla ya Corona, watoto na vijana walibeba mzigo wa matatizo ya afya ya akili bila kuwepo kwa uwekezaji wa kutosha kutatua tatizo hilo.
Utafiti wa UNICEF na Gallup katika nchi 21 umebaini kuwa kijana kati ya 1 hadi watano wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 mara nyingi walikuwa na msongo wa mawazo au hawakuwa na hamu ya kufanya kitu chochote.

“Miezi 18 ya Corona ni muda mrefu kwetu sote, hasa kwa watoto. vizuizi vya kutembea vilivyowekwa katika nchi il ikudhibiti Corona, vimefanya watoto wawe mbali na familia zao, marafiki, madarasa yao bila kusahau michezo, mambo ambayo ni ya msingi katika ukuaji wa mtoto,” amesema Henrietta Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF.
Ameongeza kuwa madhara yake ni makubwa na kinachoonekana sasa ni taswira ndogo ya hali halisi “Kwa kuwa hata kabla ya Corona, watoto walikuwa wametishwa mzigo wa matatizo ya afya ya akili ambayo hayakushughulikiwa. Fedha zinazotengwa ni kidogo na pia uhusiano kati ya afya ya akili na ustawi wa baadaye wa mtoto nao hautiliwi maanani.”
Ni kwa mantiki hiyo ripoti inapendekeza mambo muhimu matatu ya kufanywa na serikali na sekta binafsi ikiwemo; kuwekeza katika afya ya akili kwa vijana na watoto, kujumuisha hatua za kuchukua katika sekta zote iwe shuleni, nyumbani au hospitalini ili kusaidia afya njema ya akili na pia  kuvunja ukimya unaozingira magonjwa ya akili kwa kuondoa unyanyapaa dhidi ya wagonjwa na kuzingatia uzoefu wa watoto na vijana katika suala hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF anatamatisha akisema ,”afya ya akili ni sehemu ya afya ya mwili, hatuwezi kuendelea kuona vinatengeshwa. Kwa muda mrefu katika nchi tajiri na maskini tumeshuhudia uelewa mdogo au uwekezaji mdogo katika suala hili ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto. Hii lazima ibadilike.”
TAGS: UNICEF, SOWC, Afya ya Akili, COVID-19
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
2'42"
Photo Credit
IOM/Kaye Viray