Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamba ni zaidi ya kitambaa cha nguo

Pamba ni zaidi ya kitambaa cha nguo

Pakua

Leo ni siku yap amba duniani ikiwa ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku hiyo kuenzi zao ambalo kitabaa chake kinatengeneza mavazi ya kila siku kwenye mkabati mengi ya nguo ni kitambaa kizuri, rahisi kuvaa, kukitunza na kinadyumu kwa muda mrefu. Lakini kwa mujibu wa Umoija wa Mataifa pamba inawakilisha zaidi ya kitambaa kama inavyofafanua taarifa ya Flora Nducha 

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO zao hili asili ni bidhaa inayobadilisha maisha duniani linawasaidia wakulima milioni 28.67 na kuzifaidisha zaidi ya familia milioni 100 katika nchi 75 kwenye mabara 5. 

Hii inamaanisha kuwa, kwa kila vazi la pamba, ukifuatilia nyuma ya mnyororo wake wa biashara kuna hadithi ya binafsi. 

FAO inasema ni kweli kwamba pamba ni muhimu sana kwa uchumi ulioendelea, lakini kwa nchi masikini na zinazoendelea  pamba ni kimbilio na mkombozi wa maisha. 

Pamba ni chanzo kikuu cha maisha na kipato kwa wafugaji wengi wadogo  wa vijijini na vibarua, wakiwemo wanawake, kwani kilimo cha zao hilo kinatoa ajira na mapato kwa baadhi ya maeneo masikini zaidi ya vijijini duniani. Miongoni mwa wakulima hao ni María Rosa Farroñán, kutoka jamii ya watu wa asili ya Mochica nchini Peru anaelezea uzoefu wake wa kulima na kuchakata pamba. 

Anasema “Pamba asilia kutoka Peru ndio ilikuwa ya kwanza kujulikana duniani, hakukuwa na aina nyingine hapo kabla , mbegu mchanganyiko ya Pima haikuwepo wakati nakua nap amba hii ni ngumu kuchambua, sio rahisi kama mpamba ya asili ambayo uchahambua kwa haraka na kutoa mbegu sababu nil aini. Hata hivyo pamba inasusaidia sana na kuokoa maisha yetu.” 

Rosa anasema mkatato mzima kuanzia kilimo, kuchambua, kusokota n ahata kufikisha sokoni unachukua muda mrefu na kazi kubwa, lakini yeye hana kazi nyingine aipendayo kama ya kulima pamba. 

Umoja wa Mataifa unasema maadhimisho haya ya kwanza lengo lake ni kutangaza sekta yap amba na kuelimisha kuhusu jukumu kubwa ililonalo katika maendeleo ya uchumi, biashara ya kimataifa na kutokomeza umasikini. 

Wazo la kuwa na siku yap amba duniani lilizaliwa mwaka 2019ambapo nchi 4 za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara wazalishaji wakubwa wa pamba ambazo ni Benin, Burkina Faso, Chad na Mali “The cotton four” zilipopendeka kwa shirika la biashara duniani WTO Kamba tarehe 7 Oktoba iwe maadhimisho ya siku yap amba duniani.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
2'40"
Photo Credit
© FAO/Aamir Qureshi