Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FISH4ACP kunasua wavuvi na wachuuzi wa samaki Katavi nchini Tanzania

FISH4ACP kunasua wavuvi na wachuuzi wa samaki Katavi nchini Tanzania

Pakua

Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limetambulisha mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika mkoani Katavi baada ya mradi huo unaohusisha nchi 12 za Afrika, Karibea na Pasifiki kuwa na matokeo chanya kwa wavuvi mkoani Kigoma. Devotha Songorwa wa Radio washirika KidsTime FM anafafanua zaidi katika ripoti hii.

Mkoani Katavi, kusini magharibi mwa Tanzania shughuli mahsusi ni utambulishaji wa mradi wa FISH4ACP ( Fish for ACP) unaolenga kuboresha mazao ya baharini kwa lengo la kulinda mazingira na kuinua kipato cha wananchi. Walengwa ni wavuvi na mmoja wao akanieleza

Akizungumza na UN News, Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvivu na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin amesema mradi huu ulioanza kutekelezwa nwezi Septemba mwaka jana wa 2020 unagharimu zaidi ya dola milioni  46. Na vipi ujio wa mradi huu mkoa wa Katavi?

Naye Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Donald Kusekwa amebainisha kuwa kwa sasa hali ya uvuvi Wilayani Tanganyika  siyo ya kuridhisha kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kusababisha kupungua kwa dagaa na samaki hivyo kufanya wakazi wa maeneo hao kukosa kitoweo hicho na ujio wa mradi wa FISH4ACP ni mkombozi kwao na umewafika kwa wakati sahihi.

Nao baadhi ya wavuvi na wafanya biashara wakazungunzia ujio wa mradio huo na namna utakavyowanufaisha kufanya shughuli zao kuondokana na Uvuvi wa mazoea hatimaye kuvua kisasa.
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Devotha Songorwa
Audio Duration
4'27"
Photo Credit
UN Tanzania