Kufanya kazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii
Kutana na mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jason William Gbambi ambaye ni afisa uhamasishaji wa timu ya maadili na nidhamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Anasema kufanya kazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii na kutambua mahitaji yao na hasa amani ambayo ni adumu nchini humo.