Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

IOM 2018/Ahmed Badr

Msakata kabumbu mwenye asili ya Afrika atangazwa kuwa balozi mwema wa UNHCR

Kutana na balozi mwema mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, si mwingine bali ni mwana kaandanda nyota Alphonzo Davies, anayesakata gozi kwenye timu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani lakini pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Canada. Ametangazwa leo kufuatia mchango wake mkubwa kwa wakimbizi. Jason Nyakundi anatupasha zaidi

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Nattss…. 

Sauti
2'9"
© UNICEF/UN0377403/Roger LeMoyne

Nchini DRC mashirika ya UN yaendelea kuwa mkombozi kwa wakimbizi

Katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umeendelea kusambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani ambao walilazimika kukimbia makwao na kuacha kila kitu na hivi sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi hususan katika eneo la Pinga jimboni humo. Misaada hiyo imekuwa jawabu kwa wakimbizi ugenini. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Sauti
2'35"
UNAMID/Hamid Abdulsalam

UNFPA ina mchango mkubwa katika afya ya uzazi Sudan:Kanem

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA, Dkt. Natalia Kanem amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Sudan ambako pamoja na kupongeza serikali ya mpito na wananchi wake kwa maendeleo yaliyofikiwa nchini humo, ameshuhudia jinsi uwekezaji kwa wanawake na vijana kumekuwa msaada mkubwa hasa katika sekta ya afya ya uzazi. Ni kwa vipi basi? Tuungane basi na Dkt. Natalia mwenyewe katika simulizi yake inayosomwa studio na John Kibego. 

(Taarifa ya John Kibego) 

Nats… 

Sauti
2'13"
UNICEF/Mauricio Bisol

Maelfu waendelea kufungasha virago Cabo Delgado kufuatia mashambulizi:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema machafuko yanayoendelea kwenye jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji hadi sasa yamewalazimisha watu 670, 000 kushafungasha virago na kugeuka kuwa wakimbizi wa ndani huku dunia ikishindwa kuupa kipaumbele mgogoro huo. Tupate ufafanuzi zaidi kutoka kwa Jason Nyakundi 

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) 

Nattss….. 

Sauti
3'13"

19 MACHI 2021

Katika jarida hili la mada kwa kina leo Grace Kaneiya anakuletea

-Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Zlatan Milisic amempongeza Samia Suluhu Hassan kuapishwa na kuwa mwanamke wa kwanza Rais nchini Tanzania na kuahidi kushirikiana na serikali yake

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kundi la wapiganaji la ADF limekatili maisha ya watu zaidi ya 600 na kufurusha wengine 40,000 Mashariki mwa nchi hiyo.

Sauti
12'6"
UN/maktaba

UN na viongozi wengine wa dunia watoa pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais

 Kifo cha Rais wa Tanzania John Magufuli kimegusa viongozi mbalimbali ukiwemo Umoja wa Mataifa, mashirika yake na marais na hata viongozi wastaafu kama anavyosimulia Flora Nducha katika taarifa hii baada ya kurambaza kwenye mitandao ya kijamii. 

(Taarifa ya Flora Nducha) 

Salamu za hivi karibuni zaidi za rambirambi zinatoka Umoja wa Mataifa ambako Tanzania ni mmoja wa wanachama. 

Sauti
2'20"
Muhiddin Michuzi

Jumuiya ya kimataifa na viongonzi mbalimbali wamuenzi Rais Magufuli

Kifo cha Rais wa Tanzania John Magufuli kimegusa viongozi mbalimbali ukiwemo Umoja wa Mataifa, mashirika yake na marais na hata viongozi wastaafu kama anavyosimulia Flora Nducha katika taarifa hii baada ya kurambaza kwenye mitandao ya kijamii. 

(Taarifa ya Flora Nducha) 

Salamu za hivi karibuni zaidi za rambirambi zinatoka Umoja wa Mataifa ambako Tanzania ni mmoja wa wanachama. 

Sauti
4'22"
Ikulu Tanzania

Tanzania yaomboleza kwa siku 14, ni kufuatia kifo cha Rais John Magufuli

Tanzania imeanza maombolezo ya siku 14 huku bendera zikipepea nusu mlingoni kufuatia  kifo cha Rais wa nchi hiyo  Dkt. John Pombe Magufuli  kilichotokea jana saa 12 jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo. Mauti yakimkuta Rais Magufuli alikuwa na umri wa miaka 61. Flora Nducha na maelezo zaidi.
 
Mwendazake John Magufuli ameaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyoko jijini Dar es salaam ambako alilazwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. 

Sauti
5'34"