Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasema watu wasibweteke COVID-19 bado ipo ingawa vifo vimepungua

WHO yasema watu wasibweteke COVID-19 bado ipo ingawa vifo vimepungua

Pakua

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imeendelea kuongezeka kote dunini kwa wiki ya nne mfululizo huku wagonjwa milioni 3.3 wapya wakiripotiwa katika siku saba zilizopita limesema leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Ahimidiwe Olottu na taarifa zaidi

(TAARIFA YA AHIMIDIWE OLOTTU)

Kupitia shirika la kimataifa la kufanikisha uwepo wa tiba nafuu duniani, UNITAID linaloratibiwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, dawa hiyo mpya ni Rifapentine na tayari imeanza kutolewa katika nchi 5 zenye kiwango kikubwa zaidi cha TB barani Afrika ambazo ni  Ethiopia, Ghana, Kenya, Zimbabwe na Msumbiji. 

Msemaji wa UNITAID Herve Verhoosel akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswsi amesema  

(Sauti ya Herve Verhoosel) 

 “UNITAID ina furaha kuwajulisha kuhusu tiba mpya ya gharama nafuu dhidi ya Kifua Kikuu. Tiba mpya gharama yake ni nafuu kwa asilimia 70 kuliko dawa za awali. Inaitwa Rifapentine na kwa majadiliano kati ya UNITAID na wadau wake, dawa hii inaweza kupatikana katika nchi zaidi ya 100 kwa gharama ya dola 15 badala ya dola 45.” 

WHO inapendekeza matumizi ya tiba hii mpya kwa watu wagonjwa wa Kifua Kikuu kilichofikichika na ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi, VVU na wagonjwa wengine wenye Kifua Kikuu wa umri wowote.

Utafiti umebaini kuwa wagonjwa wana uwezo mkubwa wa kukamilisha matibabu katika kipindi kifupi. 

Wagonjwa wa Kifua Kikuu wanaweza kuambukiza ugonjwa huo kwa watu kati ya 10 hadi 15 wanaokaribiana nao kwa mwaka mzima ambapo UNITAID inasema bila tiba sahihi, asilimia 45 ya watu wasio na VVU wenye Kifua Kikuu na watu wenye VVU na Kifua Kikuu wanaweza kufariki dunia. 

Inakadiriwa kuwa mwaka 2019, watu wapatao milioni 10 waliambukizwa Kifua Kikuu, idadi ambayo imekuwa ikipingua taratibu mno katika miaka ya karibuni. Katika idadi hiyo milioni 5.7 ni wanaume, milioni 3.2 wanawake na milioni 1.1 ni watoto na idadi kubwa wanaishi katika nchi za kipato cha chini na kati. 

Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 nalo limekuwa mwiba katika tiba dhidi ya kifua kikuu kwa kuwa linavuruga utoaji wa huduma za Kifua Kikuu. 

Hata hivyo Bwana Veroosel amesema kutokana na tiba hii mpya, zaidi ya wagonjwa milioni 3 wanaweza kupatiwa tiba hii mwaka huu wa 2021. 

 

Audio Duration
2'32"
Photo Credit
University of Oxford/John Cairns