UNFPA ina mchango mkubwa katika afya ya uzazi Sudan:Kanem

UNFPA ina mchango mkubwa katika afya ya uzazi Sudan:Kanem

Pakua

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA, Dkt. Natalia Kanem amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Sudan ambako pamoja na kupongeza serikali ya mpito na wananchi wake kwa maendeleo yaliyofikiwa nchini humo, ameshuhudia jinsi uwekezaji kwa wanawake na vijana kumekuwa msaada mkubwa hasa katika sekta ya afya ya uzazi. Ni kwa vipi basi? Tuungane basi na Dkt. Natalia mwenyewe katika simulizi yake inayosomwa studio na John Kibego. 

(Taarifa ya John Kibego) 

Nats… 

Ni Dkt. Natalia Kanem huyo akisema “tunahitimisha siku nzuri, tukiwa na jamii za jimbo la Blue Nile ambapo nilipotembelea jamii inayoishi kwenye mahema nimekutana na Aziza.” 

Mkuu huyu wa UNFPA akiwa na Aziza anasema “Aziza ni mwanamke wa kijijini aliyeelimika, aliyekimbia makazi yake ya awali na sasa anaishi Shanisha. Ndoto ya Aziza na kile apendacho zaidi kufanya ni kuwa mwalimu wa shule ya chekechea.” 

Dkt. Kanem anasema alikutana pia na wanawake wengine wa kijijini wenye uwezo mkubwa. 

Akionekana akiwa na wanawake hao, Dkt. Kanem anasema kile kilichomgusa zaidi ni vile ambavyo wamejipanga kwenye usimamizi wa fedha, kwa lengo la kuweza kupatia usafiri wajawazito. 

Nats.. 

Anasema mwanamke yoyote aliye hatarini kupoteza maisha wakati wa kujifungua anapatiwa fedha ili aweze kwenda kliniki ya kijamii na hospitali niliyotembelea ilikuwa mfano mzuri wa jins UNFPA inaokoa maisha, hata wakati ambapo huduma ya upasuaji kwenye uzazi inahitajika chini ya mazingira magumu. 

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyu wa UNFPA anasema sehemu bora zaidi ya ziara yake ni pale alipokabidhi funguo ya baiskeli ya magurudumu matatu ambayo hutumika kama gari la wagonjwa. 

Nats.. 

“Baiskeli hii inaitwa Tuk Tuk hapa Sudan na kukabidhi funguo kwa mwanamke thabiti kwenye jamii hii, lilikuwa jambo la kufuruhisha zaidi.” 

Nats.. 

Na zaidi ya yote ni kuona machifu, watoto, wakunga na wafanyakazi wote wa UNFPA wakiwa pamoja kuhakikisha tunafanikisha lengo la afya. Na hii ndio sababu ya kufanya hivi na ilikuwa siku nzuri.. 

Nats.. 

 

Audio Duration
2'13"
Photo Credit
UNAMID/Hamid Abdulsalam