Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 MACHI 2021

19 MACHI 2021

Pakua

Katika jarida hili la mada kwa kina leo Grace Kaneiya anakuletea

-Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Zlatan Milisic amempongeza Samia Suluhu Hassan kuapishwa na kuwa mwanamke wa kwanza Rais nchini Tanzania na kuahidi kushirikiana na serikali yake

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kundi la wapiganaji la ADF limekatili maisha ya watu zaidi ya 600 na kufurusha wengine 40,000 Mashariki mwa nchi hiyo.

-Huko Myanmar vikosi vya usalama vimeelezwa kuendelea kusababisha madhila kwa wananchi baada ya kuvamia shule takriban 65 kuua na kujeruhi waalimu , UNICEF, UNESCO na save the Children wamesema leo wakihofia elimu kuvurugwa zaidi

-Na katika mada kwa kina leo tunazungumza na balozi Getrude Mongella aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing miaka 25 iliyopita nchini Beijing China alifafanua kuhusu wanawake na uongozi

-Na leo tunajifunza Kiswahili tutakuwa Kenya kujifunza methali "Mui huwa mwema" na mchambuzi wetu ni Josephat Gitonga, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika kituo cha tafsiri na ukalimani .

 

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
12'6"