Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwaenzi waathirika wa utumwa kwa kutokomeza misingi yake inayoendelea leo hii:UN

Tuwaenzi waathirika wa utumwa kwa kutokomeza misingi yake inayoendelea leo hii:UN

Pakua

Katika siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashata ya utumwa katika bahari ya Atlantiki hii leo Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ili kuwaenzi vyema mamilioni ya watu wenye asili ya Afrika waliopitia madhila asiyoelezeka katika utumwa na biashara ya utumwa ni vyema kuyania wazi yaliyowasibu na kuhakikisha yatokomezwa.

Katika ujumbe wake wa siku hii Antonio Guterres amesema

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

“Biashara hii iliunda na kudumisha mfumo wa unyonyaji ambao uliokuwepo kwa zaidi ya miaka 400, ukisambaratisha familia, jamii na uchumi. Tunakumbuka kwa unyenyekevu mnepo wa wale waliovumilia unyama uliofanywa na wafanyabiashara na wamiliki wa watumwa, na kuenziwa na wafaidika wa utumwa. Tunatambua michango mikubwa iliyowafanya na watumwa wanaume, wanawake na watoto katika utamaduni, maarifa na uchumi wa nchi walizopelekwa.” 

Ameongeza kuwa leo hii tunawaenzi waathirika wa biashara hiyo ya utumwa kwa kuelimisha kuhusu historia yao na kutambua athari za biashara hiyo katika ulimwenghu wa sasa kwa sababu

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

“Biashara ya watumwa ya bahari ya Atlantiki ilimalizika zaidi ya karne mbili zilizopita, lakini fikra za kuwaona wazungu ni bora kuliko wengine zilizokuwa kichocheo wakati huo bado ziko hai. Lazima tuutokomeze urithi wa uwongo huu wa kibaguzi. Lazima tufanyekazi pamoja kushughulikia athari mbaya na zinazoendelea za utumwa na biashara ya watumwa ya Atlantiki. Na tutafanya hivyo tu kwa kuongeza ari yetu ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi, ukosefu wa haki na usawa na kwa kujenga jamii na uchumi shirikishi.” 

 

 

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
1'38"
Photo Credit
UN Photo/Devra Berkowitz