Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi kutoka Syria: Ovale Citoyen ya Ufaransa wamenirudisha michezoni.

Mkimbizi kutoka Syria: Ovale Citoyen ya Ufaransa wamenirudisha michezoni.

Pakua

Nchini Ufaransa, wanamichezo wa zamani wataalamu wa mchezo wa raga, kupitia taasisi yao ya Ovale Citoyen, wanatumia mchezo huo kama njia ya kujenga kujiamini na kuleta hali ya kijamii kati ya wakimbizi na watu waliotengwa. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Houssam anajitambulisha kuwa yeye ni raia wa Syria na ana umri wa miaka 35. Anasema nchini Syria alikuwa mwanahabari, na kabla ya hapo alikuwa mwanamichezo mwenye ushindani na mara tatu alikuwa mshindi wa kitaifa wa ngumi na mateke. Kisha alipopigwa risasi ya kifua alifikiri huo ndio ulikuwa mwisho wake katika michezo lakini kumbe hakujua kuwa baadaye mambo yangekuwa tofauti.

Akiwa ukimbizini nchini Ufaransa akafahamu kuhusu uwepo wa Ovale Citoyen, chama cha mchezo wa raga kinachoendeshwa na wataalam wa zamani wa mchezo huo.  "Nilipofika Ufaransa, niliigundua Ovale Citoyen. Walinitia moyo nirudi kwenye michezo. Walinisaidia kupata nguvu ya kuendelea. Rugby imekuwa muhimu sana kwangu. Ilinipa mawasiliano na jamii. Ilinipa mawasiliano na marafiki wapya. Ilinipa fursa za kazi, na nafasi ya kuanza maisha yangu tena. Vitu vingi. Na muhimu, ilinipa matumaini.” 

Jeff Puech ni Mwanzilishi wa Ovale Citoyen, anasema,  “Ovale Citoyen ni kilabu ya raga na mpira wa miguu yenye mpango maalumu wa kijamii. Inahusu ujumuishaji, na kusaidia mtu yeyote anayekabiliwa na ubaguzi kupata utu, kazi, na ujumuishaji halisi wa kijamii. " 

Audio Credit
Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
1'55"
Photo Credit
Screenshot