Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto ya mtoto mkimbizi kuwa daktari yawezeshwa na UNICEF.

Ndoto ya mtoto mkimbizi kuwa daktari yawezeshwa na UNICEF.

Pakua

Nchini Niger watoto wakimbizi waliolazimika kukimbia Libya kutokana na ghasia za ugenini hivi sasa wanaona nuru ya maisha yao baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF, kuwapatia maeneo salama siyo tu ya kucheza bali pia kujifunza.  Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Miongoni mwa watoto hao ni Wichah Nasradine, mtoto mwenye uraia wa Sudan, akiwa Agedez nchini Niger, na ana umri wa miaka 13. 

Wichah hivi sasa yuko ukimbizini kwenye nchi ya tatu, Niger akisema, “tulikimbia nchi yetu Sudan kwa sababu ya vita. Tulikimbilia Libya, ambako nako tumekimbia kwa sababu ya vita. Nchini Libya tulisikia milio mizito ya risasi. Mama yetu alituficha nyumbani. Tuliwasili hapa Niger mwaka 2018 ili kusaka hifadhi. Ili kusahau vita tunatoka kucheza nje, nacheza pia na kaka zangu.” 

Wichah ambaye ana ndugu wanne ambao ni kaka na dada zake, anasema siku moja walitaka mtoto mmoja mwakilishi wa watoto, na ndipo walimchagua yeye. 

Wichah anakwenda shuleni na anasema yeye ni mwakilishi kwa hiyo huzungumzia elimu kwa kuwa shule ni muhimu na ndio ufunguo ambao unaweza kutumia kufungulia kila kitu maishani.  Mtoto huyu anaendelea kusema kuwa darasani wana mwalimu mmoja anayewafundisha lugha ya kifaransa. 

Tayari Wichah ameandikishwa darasa la kwanza na anasema ya kwamba, “shuleni kwake ana marafiki kutoka Niger amao wanasoma na kucheza pamoja.” 

Na zaidi ya yote, Wichah ana ndoto na anasema “nikiwa mkubwa nataka kuwa daktari ili niweze kutibu wagonjwa.” 

Kwa mujibu wa UNICEF, vita vya wenyewe kwa wenyewe vimefurumusha zaidi ya watoto milioni 30. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
2'
Photo Credit
© UNICEF/Juan Haro