Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawa ya kulevya huathiri sehemu ya ubongo iliyo karibu na sikio- Daktari

Madawa ya kulevya huathiri sehemu ya ubongo iliyo karibu na sikio- Daktari

Pakua

Leo ni siku ya kimataifa ya mapambano dhidi ya matumizi na usafirishaji haramu wa mihadarati. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni haki kwa ajili ya afya na afya kwa ajili ya haki. Katika mahojiano yangu ya awali kwenye studio zetu za hapa mjini New York, na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo, Dokta Juma Magogo Mzimbiri aliyeko masomoni hapa Marekani amenieleza mihadarati inafanya nini ikiingia katika ubongo wa binadamu akifafanua kuwa, “tatizo hili la mihadarati linaathiri sana sehemu ya ubongo ambayo iko kwa ndani karibu kabisa na sikio. Na hapo kuna sehemu ya ndani zaidi ambayo inahusika na kazi tofautitofauti ikiwemo kuhifadhi kumbukumbu za muda mfupi uliopita, utambuzi wa hisia kama vile kufurahi au kusikitika, sasa tatizo la mihadarati linakuja pale ambapo linaingilia mfumo huu unashindwa kufanya kazi inavyotakikana.”

Na ni kwa nini watumiaji wa madawa ya kulevya huongeza kiwango cha dawa kadri muda unavyosogea? Dkt. Mzimbiri anasema kwamba, “kikubwa ni kwamba athari za mihadarati zinakuwa zinaongezeka siku baada ya siku. Kwa kadri kile kiwango alichokuwa anakihitaji ili kupata furaha, baada ya muda kinaongezeka na hivyo atahama kutoka kete moja na baadaye mbili, tatu na ataendelea kuongeza na kuongeza wakati huo akiongeza athari kwenye mwili siyo tu kwenye ubongo, na viungo vingine vinaathirika.”

 

 

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
2'14"
Photo Credit
UNAMA/Najeeb Farzad