Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Ban alaani mauaji ya mlinda amani wa UM nchini DRC

Imebainika kuwa mlinda amani aliyeuawa Jumatatu asubuhi huko Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kutoka Afrika Kusini.

Kufuatia taarifa hizo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mauaji hayo yaliyofanyika wakati wa makabiliano kati ya askari wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa DRC, MONUSCO na wapiganaji wanaosadikiwa kuwa wa Mai-Mai.

Katika makabiliano hayo walinda amani wengine wawili wa Afrika Kusini walijeruhiwa.

UNESCO na kongamano la sayansi endelevu.

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linafanya kongamano kuhusu matumizi ya sayansi endelevu mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia, lililoanza leo Desemba 19 hadi Desemba 21.

Lengo kuu la mradi huo ni kwa ajili ya kukuza mjadala na kusambaza ujumbe wa sera thabiti  ambayo itasaidia nchi wanachama wa UNESCO kuanzisha mbinu za sayansi katika kukabiliana na changamoto kote duniani. Na kuendeleza seti ya miongozo kutoka kwa ufafanuzi katika mwisho wa 2017.

Kazi za Umoja wa Mataifa nchini Uganda kwa mwaka huu wa 2016

Umoja wa Mataifa  umejikita nchini Uganda katika shughuli kadhaa za usaidizi wa masuala ya kibinadamu pamoja na miradi ya maendeleo, ambapo mashirika kadhaa kama vile shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mpango wa chakula WFP, la kuhudumia watoto UNICEF nakadhalika yamejikita humo.

Miongoni mwa mambo makuu yanayofanywa na umoja huo ni usaidizi kwa malefu ya wakimbizi kutoka nchi jirani ambazo zimekumbwa na machafuko ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Burundi na Sudan Kusini.

UN Photo/Eskinder Debebe)

Aleppo ni kisawe cha Jehanam, na jamii ya kimataifa imeshindwa- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amefanya mkutano rasmi wa mwisho na waandishi wa habari mjini New York ikiwa ni takribani majuma mawili kabla ya kumaliza awamu ya pili na ya mwisho ya uongozi wake katika chombo hicho .

Katibu Mkuu amezungumzia mambo mseto ambayo Umoja wa Mataifa unayatekeleza  na yaliyokumbwa na changamoto ikiwemo Syria. Amesema suala la Aleppo linamsikitisha sana kwani raia wanauawa, kutoka kwao  inakuwa ni shida huku akifananisha Aleppo na Jehanam.

UN Photo/Eskinder Debebe)

Dola milioni 241 zaombwa kusaidia wakimbizi bonde la ziwa Chad

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amezindua ombi la dola milioni 241 ili kusaidia zaidi ya watu nusu milioni waliokwana huko Niger, Chad na Cameroon kutokana na mashambulizi ya Boko Haram kwa mwaka ujao wa 2017.

Uzinduzi huo umefanyika huko Yaounde Cameroon ambako fedha hizo zinalenga kusaidia pia zaidi ya wakimbizi 183, 000 kutoka Nigeria.

Misri acheni kukandamiza watetezi wa haki wanawake- Wataalam  

Kundi la wataalam maalum wa Umoja wa Mataifa hii leo wamelaani vikali Misri kwa kitendo cha kutumia msako wao dhidi ya mashirika ya kiraia kukandamiza wanawake watetezi wa haki za binadamu na makundi yanayotetea haki za wanawake .

Hii ni kwa mujibu ya taarifa yao kutoka Geneva, Uswisi ambapo wataalamu hao wamesema hatua ya serikali inawazuia wanawake watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zao halali ambapo maelfu ya wanawake wanahitaji usaidizi na usalama

UNAMID yahofia wafanyakazi wa zamani kukwamisha operesheni

Ujumbe wa pamoja Muungano wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID huko Darfur hii leo umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya majaribio ya hivi karibuni ya mara kwa mara ya wafanyakazi wa zamani wa ujumbe huo ya kutaka kuvuruga operesheni zake.

Taarifa UNAMID imesema kuwa kwa mara kadhaa wafanyakazi kazi hao wamekuwa wakizuia operesheni ndani ya nje ya kambi na wakati mwingine kuzuia wafanyakazi wa UNAMID ambao ni raia wa Sudan kuingia kwenye maeneo ya kazi zao.

Ulimwengu washuhudia kuporomoka kwa mishahara-ILO

Shirika la Kazi Duniani, ILO limesema kiwango cha mshahara katika nchi zilizoibuka kiuchumi au G20 kimeshuka au kudorora kutoka asilimia 6.6 mwaka 2012 hadi asilimia 2.5 mwaka 2015, na hii imeathiri zaidi ukuaji wa mishahara ulimwenguni kote.

Ripoti ya ILO iitwayo "Ripoti ya Kimataifa ya Mshahara ya mwaka 2016-2017" ambayo imetolewa leo imeonyesha kuwa kiwango cha ukuaji wa mshahara ulimwenguni kimeshuka na kufikia asilimia 1.7, kiwango ambacho ni cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika miaka minne.

Hakuna mikono salama kwa silaha za maangamizi- Eliasson

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu azimio namba 1540 la  kuzuia janga lisababishwalo na matumizi ya kiholela ya silaha za maangamizi ya umma.

Mjadala huo umejikita kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa katika  kuzuia matumizi ya kiholela ya silaha hizo kunakofanywa na vikundi visivyo vya kiserikali, teknolojia mpya na vitisho vipya katika suala hilo.