Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

World Bank

Sekta ya tumbaku tumia mitandao ya kijamii kwahitaji mpango wa kiamataifa:WHO

Matumizi ya tovuti kuchagiza uraibu kama wa sigara yametajwa kama moja ya changamoto kubwa katika juhudi za kimataifa za kupunguza uvutaji sigara wamesema wataalamu wa afya wa Umoja wa Mataifa Jumatatu.

Katika wito wa kuchukua hatua kabla ya mkutano wa kimataifa wa udhibiti wa bidhaa za tumbaku , shirika la afya duniani WHO limesema, nchi ni lazima zishirikiane kufuatilia matangazo hoyo kila pembe duniani.

Hakuna mshindi mgogoro Yemen: UM

Umoja wa Mataifa umewahakikishia viongozi wa kisiasa nchini Yemen , kuwa hakuna mshindi katika mgogoro unaofukuta nchini humo na kulitaka taifa hilo kukubali mpango wa mchakato wa amani.

Mchakato wa awali wa kusaka amani nchinio humo haujazaa matunda.

Akiongea wakati wa mkutano wa baraza la usalama, ulioangazia hali mashariki ya kati hususani Yemen , mwakilishi maalum wa UM nchini humo Ould Cheikh Ahmed amesema.

(SAUTI AHMED)

Uchumi wa Kenya kukua kwa 6% mwaka 2017-Benki ya Dunia

Uchumi wa Kenya unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2016 kutoka asilimia 5.6 mwaka 2015 imesema leo ripoti ya kiuchumi ya Benki Kuu ya dunia.

Kulingana na ripoti hiyo ukuaji wa uchumi wa Kenya umeendelea kuimarika katika kipindi cha miaka minane iliyopita na hali hii inatarajiwa kuendelea katika nusu ya mwaka, huku ukuaji uchumi ukitarajiwa kupita asilimia 6 mwaka 2017 na 2018.

Watu milioni 5 wakabiliwa na njaa Somalia:WFP

Zaidi ya watu milioni tano nchini Somalia hawana chakula cha kutosha, na zaidi ya milioni moja kati yao wanahitaji msaada wa kuokoa maisha, amesema mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Somalia.

WFP na washirika wake wanaongeza juhudi za kuzisaidia jamii kukabiliana na ukame mkali uliosababishwa na El Niño. Uwezo wa jamii hizo ambazo zimekumbana na misimu minne ya ukosefu wa mvua umefika kikomo.

Mkuu wa WFP Somalia Laurent Bukere anaelezea hofu yake kuhusu kupungua kwa uhakika wa chakula na nini ofisi yake inafanya kuepuka janga kubwa la kibinadamu.

Wakimbizi wa ndani wazidi 15,000 Mosul, Iraq: UNICEF

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa leo Ijumaa, idadi ya watu wanaokimbia makazi yao kaskazini mwa Iraq ni zaidi ya 15,000 katika siku kumi za operesheni ya jeshi la usalama la Iraq kuchukua mji wa Mosul. Wengi wanakimbilia vijiji vingine kwa jamii ambazo pia wanajikuta mashakani mashaka.

UN Photo/Amanda Voisard

Kujitioa ICC sio sahihi: Ban

Tamko la nchi tatu za Afrika la kujitoa kwenye mkataba wa mahakama ya kimataifaya uhalifu ICC, linatuma ujumbe mbaya amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akiongea na wajumbe wa baraza la usalama Ijumaa, Ban amesema kujitoa kwa Afrika Kusini, Gambia na Burundi kwa uanachama kunaathiri majukumu ya uketekezaji wa haki.

Amesema kupitia mahakama hiyo dunia imepiga hatua kubwa katika mfumo wa sheria ambayo imetoa usalama dhidi ya uhalifu bila kuchukuliwa hatua.