Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN Photo/Loey Felipe

Harakati za Fatah zimegeuza wakimbizi kuwa jasiri: Mladenov

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov amezungumza huko Ramallah, wakati wa siku ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina akipongeza kikao cha Saba cha kikukndi cha Fatah kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa wapalestina.

Amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa wawe na maazimio ambayo yatahakikisha utambuzi wa mwelekeo wa watu wa Palestina kwa ajili ya kutimiza haki zao za kujitawala, kusaka taifa, heshima na uhuru.

Picha: PAHO/WHO/D Spitz

UM watangaza dola milioni 400 kutokomeza kipindupindu Haiti

Umoja wa Mataifa leo umetangaza kiasi cha dola milioni 400 kwa kipindi cha miaka miwili ambacho kitatumiwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, ametoa tangazo hilo akisema mkakati huu mpya dhidi ya kipindupindu ulitangazwa mwezi Agosti mwaka jana na utawasilishwa kwa Katibu Mkuu Desemba mosi mwaka huu ambapo unahusiaha maeneo hatua za haraka katika maeneo ambapo matukio yameripotiwa na kusababaisha migogoro ya afya ya umma.

Kila mtu anastahili huduma na ulinzi dhidi ya Ukimwi: Ban

Kwaya maalum ikihamasisha kuhusu makabiliano dhidi ya ukimwi katika tukio maalum hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Katika hotuba yake wakati wa tukio hilo la siku ya ukimwi duniani ambayo itaadhimishwa kesho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema makabiliano dhidi ya ukimwi ni muhimu kwa kuwa kila mtu anastahili matibabu na makundi hatarishi yote yanastahili ulinzi dhidi ya unyanyapaa na ukatili.

Ukabila, ulemavu na mrengo wa siasa waengue watu kwenye huduma- Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imezinduliwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ikisema kuwa katika miongo iliyopita ustawi wa binadamu umepata mafanikio ya aina yake, umaskini ukipungua na afya za watu zikiimarika.

Ikipatiwa jina Ripoti ya hali ya kijamii duniani, umuhimu wa kumjumuisha kila mtu, ripoti hiyo hata hivyo inasema mafanikio hayo hayana uwiano, baadhi ya maeneo yakikumbwa na tofauti za kiuchumi na kijamii miongoni mwa jamii, baadhi ya wananchi wakikumbwa na vikwazo vya kusonga mbele.

Maandishi 11 mapya yaongezwa kwenye orodha ya turathi za tamaduni: UNESCO

Maandishi mapya 11 leo yameongezwa kwenye orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za Kibinadamu za shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamasduni UNESCO.

Uamuzi huo umefikiwa leo mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye mkutano ulioandaliwa na serikali na UNESCO utakaomalizika Desemba pili. Maandishi hayo yamekidhi vigezo ikiwa ni pamoja na ufahamu wa umuhimu wake katika jamii.

Uganda iko tayari kuongeza kasi ya vita dhidi ya Ukimwi

Mkurugenzi wa timu ya kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS, Bi Sheila Tlou, amezuru Uganda ili kuchagiza hatua za kushughulikia mwenendo wa ongezeko la maambukizi mapya ya ukimwi nchini humo.

Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS, kuna maambukizi mapya 360 kila wiki Uganda miongoni mwa wasichana vigori na wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15-24.

Uganda imetajwa kama moja ya nchi ambazo zinaweza kuleta mabadiliko ya kasi duniani ambayo yatachangia kukomesha ukimwi kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030.

UN Photo_JC McIlwaine

Kero kwa watoa misaada Sudan Kusini zikome: OCHA

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Eugene Owusu anawasiwasi mkubwa na mfululizo wa hivi karibuni wa kero, ukiritimba na vikwazo vinavyowakabili watoaji misaada ya kibinadamu nchini humo.

Amesema matukio 91 wakati wa utoaji misaada yamerokodiwa kuanzia tarehe 1-28 Novemba, baadhi yake ikiwa ni matukio 64 ya unyanyasaji dhidi ya wafanyakazi wa kibinadamu na mali, 18 yakiwa ni kuingiliwa kati kwa hatua na masuala ya kiutawala, 2 zikiwa ni wafanyakazi kufukuzwa kazi.

Ukatili na ubaguzi dhidi ya LGBT utokomezwe: UM

Hatua tano muhimu zinahitajika ili kukomesha ukatili na ubaguzi dhidi ya jamii ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia au LGBT, kote duniani.

Wito huo umetolewa na mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu LGBT unaofanyika nchini Thailand. Hatua hizo kwa mujibu wa Vitit Muntarbhorn ni pamoja na kuondoa sheria zinazowaathiri wasagaji, mashoga, wanaofanya mapenzi na watu wa jinsia zote mbili na waliobadili jinsia (LGBT), na kutowaona watu wa jamii inayosumbuliwa na ugonjwa.

UN Photo/Mark Garten)

Bado kuna nafasi ya kuivuta Yemen kutoka ukingoni: Ould Cheikh

Tangazo la Ansar Allah na chama cha siasa cha kongresi juu ya kuundwa kwa serikali mpya huko Yemen ni kikwazo kipya wakati huu wa mchakato wa amani na kwa maslahi ya watu wa nchi hiyo nyakati hizi ngumu.

Amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed katika taarifa yake ya leo akisema kuwa kitendo kama hicho hakitahamasisha amani.