Uwepo wa mabomu ya ardhini bado ni tishio kubwa kwa maisha ya watu Afghanistan:UNAMA
Kuwepo kwa mabomu na vifaa vingine vya mlipuko nchini Afghanistan bado ni tishio kubwa kwa maisha na vipato vya maelfu ya raia wa nchi hiyo.
Kuwepo kwa mabomu na vifaa vingine vya mlipuko nchini Afghanistan bado ni tishio kubwa kwa maisha na vipato vya maelfu ya raia wa nchi hiyo.
Safari ya kutafuta mbinu za kumsaidia mwanae ndio ilikuwa chanzo cha Dkt. John Maina kusomea elimu maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu. Dkt.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesisitiza umihimu mkubwa wa mashauriano na ushirikiano wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kufanikisha mkutano wa masuala ya kibinadamu, ambao utafanyika siku 50 tokea leo Aprili nne, jijini Istanbul, Uturuki.
Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA na serikali ya Brazil wametia saini makubaliano hii leo yenye lengo la kuimarisha hatua za usalama wa nyuklia kwa ajili ya mashindano ya michezo ya olimpiki na olimpiki ya watu wenye ulemavu itakayofanyika Rio de Janeiro baadaye mwaka huu.
Mwezi Machi shirika la mpango wa chakula duniani WFP limezindua mpango wa mlo mashuleni ambao unawasaidia watoto wa Lebanon na Syria 2wanaohudhuria shule za msingi za umma nchini Lebanon.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuudumia wakimbizi UNHCR sio sehemu ya muafaka kati ya Uturuki na Muungano wa Ulaya wa kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ugiriki hatua ambayo imeanza kufanya kazi.
Walinda amani wa Tanzania wanaotuhumiwa na ukatili na unyanyasaji wa kingono huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wamezuiliwa kambini wakati uchunguzi dhidi ya tuhuma zao ukisubiriwa.
Usonji ni tatizo ambalo linakumba jamii nyingi lakini katika nchi zinazoendelea kuna changamoto nyingi hususani kwa familia zenye watoto wenye usionji, ikiwemo kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa jamii kuelewa tatizo hilo,lakini pia unyanyapaa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa makazi, UN-Habitat, limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Dame Zaha Hadid, ambaye alikuwa mmoja wa wasanifu majengo mashuhuri zaidi duniani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha matokeo ya mkutano wa nyukilia wa mwaka 2016 mjini Washington Marekani, akipongeza tamko lililopitishwa na nchi shiriki pamoja na mpango mkakati katika kusaidia Umoja wa Mataifa.