Idadi kubwa ya watoto wenye usonji inapaswa kuwa msukumo tosha kuwasaidia:Dkt. Maina

Idadi kubwa ya watoto wenye usonji inapaswa kuwa msukumo tosha kuwasaidia:Dkt. Maina

Pakua

Safari ya kutafuta mbinu za kumsaidia mwanae ndio ilikuwa chanzo cha Dkt. John Maina kusomea elimu maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu. Dkt. Maina ambaye ni mkuu wa programu ya utafiti katika shule ya Boston Higashi ilioko jimbo la Massachusetts nchini Marekani alizungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii punde tu baada ya kuhutubia kikao cha kuadhimisha siku ya usonji kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Hapa anaanza kwa kuelezea safari yake kugundua kwamba mwanae alikuwa na usonji

Photo Credit
Dkt. John Maina (wa Tatu kutoka kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho. (Picha:UN/Rick Bajornas)