Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yazindua mpango wa mlo mashuleni kusaidia watoto wa Lebanon na Syria

WFP yazindua mpango wa mlo mashuleni kusaidia watoto wa Lebanon na Syria

Pakua

Mwezi Machi shirika la mpango wa chakula duniani WFP limezindua mpango wa mlo mashuleni ambao unawasaidia watoto wa Lebanon na Syria 2wanaohudhuria shule za msingi za umma nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa wa WFP nchini Lebanon Dominik Heinrich elimu ni muhimu saana katika kuwawezesha vijana wa Lebanon na Syria kuwa na nyenzo ambzo wanahitaji ili kuchangia katika ukanda wao hasa katika wakati huu wa matatizo.

Ameongeza kuwa kuwapa watoto hao lishe inayohitajika shuleni WFP itahakikisha lishe bora kwa watoto hao lakini pia kuwachagiza wazazi wao kuwapeleka watoto shule kila mara.

Mlo huo ni pamoja na maziwa ya kopo, maji ya matunda, vitafunwa ambavyo vinatengezezwa hapohapo Lebanon, na vipande vya matunda. Vitu ambavyo vitawatia nguvu inayohitajika na wanafunzi hao kuweza kujifunza na kufaidika na elimu.

Photo Credit
Usambazaji wa msaada wa chakula kwa watoto.(Picha:WFP/Dina El Kassaby)