Tanzania inadai maili 350 katika bahari ya Hindi
Tanzania imewasilisha ombi la kuongeza eneo la maili 150 hadi 200 za eneo lililo chini ya udhibiti wake kwenye bahari ya Hindi.
Tanzania imewasilisha ombi la kuongeza eneo la maili 150 hadi 200 za eneo lililo chini ya udhibiti wake kwenye bahari ya Hindi.
Nchi saba zitumiazo maji ya mto Nile, miaka michache iliyopita zilianzisha mkataba mpya unaotaka kuwepo kwa uwiano sawa wa matumizi ya maji ya mto Nile.
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhamiaji Shirika la kimataifa uhamiaji IOM linasema kwamba ukosefu wa huduma za matibabu kwa wahamiaji ni jambo ya kutisha na ina inahitaji kushughulikiwa kwa dharura . Jumbe Omari Jumbe wa shirika la IOM anafafanua amezungumza na Radio ya U
Ni bayana kwamba watu walemavu huwa wanapitia chamgomoto nyingi za kimaisha zikiwemo umaskini, ajira, ndoa na kusafiri kutoka eneo moja hali lingine.
Katika siku ya ukimwi duniani wito umetolewa kwa kila mtu kubeba jukumu la kujilinda na kuwalinda wengine na maambukizi mapya ya ukimwi.
Wananchi milioni 32 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshiriki hii leo katika uchaguzi mkuu ulioshuhudia wagombea 11 wakiwania wadhifa wa urais akiwemo rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila na mpinzani wake mkuu Etienne Tchisekedi.
Wakati ripoti ya shirikika la Umoja wa Mataifa la kupambana na HIV na ukimwi UNAIDS iliyotolewa leo imesema ingawa maambukizi mapya yamepungua na vifo vitokanavyo na ukimwi vimepungua lakini matunzo kwa waathirika la lishe ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya wagonjwa.
Mamia ya wakimbizi ambao walihama makwao kutokana na mzozo wa uchaguzi ulioikumba Ivory Coast wameanza kurejea nyumbani kwa usaidizi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.
Shirikisho la kimataifa la maradhi ya Kisukari IDF na shirika la afya duniani WHO wanasema maradhi ya kisukari yanaweza kuzuuilika kwa watu kuzingatia masharti ikiwemo kula vyakula vinavyofaa, kufanya mazoezi, kupungza unene na kuepuka matumizi ya tmbaku.
Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limezindua ripoti ya maendeleo ya binadamu mwaka 2011 nchini Tanzania. Washirika mbali mbali walihudhuria mkutano huo wakiwemo Dr Paniel Lyimo, katibu mkuu wa kudumu kwenye ofisi ya waziri mkuu wa Tanzania ambaye alikuwa mgeni rasmi, Dr.