UNESCO yasaidia kutoa mafunzo kwa wanahabari Yemen
Nchini Yemen, sekta ya uandishi wa habari inakabiliwa na changamoto nyingi, hususan wakati huu ambapo mgogoro wa kisiasa bado unatokota nchini humo. Waandishi nchini humo wanafanya kazi katika mazingira magumu, changamoto kubwa zaidi ikiwa ni usalama wao.