Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya afya na elimu viko hatarini Afghanistan: UNAMA/UNICEF

Huduma ya afya na elimu viko hatarini Afghanistan: UNAMA/UNICEF

Pakua

Watoto nchini Afghanistan zaidi na zaidi wanataabika kupata fursa za huduma za afya na elimu, imesema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.

Ripoti hiyo iitwayo “elimu na huduma za afya hatarini" inatanabaisha mwenendo na masuala yanayoathiri fursa za watoto kupata huduma za afya na elimu nchini Afghanistan.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja na Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan UNAMA na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF inaorodhesha jinsi gani ghasia zinazoambatana na vita, na vitisho kutoka pande zote za mgogoro vimeathiri wafanyakazi wa sekta ya afya na elimu, vimepunguza huduma, fursa za watoto kupata elimu na huduma za afya.

Ripoti hiyo imejikita katika miaka mitatu kuanzia Januari Mosi 2013 hadi 31 Desemba 2015.

Photo Credit
Mtoto wa miaka mitatu na mama yake, Kaskazini mwa Afghanistan. Picha ya UNICEF/Zalmai Ashna