Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yasaidia kutoa mafunzo kwa wanahabari Yemen

UNESCO yasaidia kutoa mafunzo kwa wanahabari Yemen

Pakua

Nchini Yemen, sekta ya uandishi wa habari inakabiliwa na changamoto nyingi, hususan wakati huu ambapo mgogoro wa kisiasa bado unatokota nchini humo. Waandishi nchini humo wanafanya kazi katika mazingira magumu, changamoto kubwa zaidi ikiwa ni usalama wao.

Kutokana na mazingira hayo, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, liliandaa hivi karibuni warsha ya mafunzo kwa wanahabari wa Yemen, chini ya mamlaka yake ya kuendeleza uhuru wa kujieleza na upatikanaji taarifa.

Hii ni katika sehemu ya juhudi zinazoendelea za kusaidia vyombo vya habari nchini Yemen kutenda kazi ya kuendeleza amani na mazungumzo, na kupasha habari kuhusu hali ya kibinadamu. Kupata picha halisi na muktadha wa mafunzo hayo, ungana na Joshua Mmali katika makala hii

Photo Credit
Mafunzo wakati wa warsha iliyoandaliwa na UNESCO.(Picha:UNESCO/Video capture)