Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2014-2016

Kutoka kushoto: Dereva wa ambulensi akisafishwa baada ya kubeba watuhumiwa wa Ebola; Jökulsárlón Glacier Lagoon huko Iceland inazidi kuwa kutoka kwa barafu inayopungua
UN Photo.
Kutoka kushoto: Dereva wa ambulensi akisafishwa baada ya kubeba watuhumiwa wa Ebola; Jökulsárlón Glacier Lagoon huko Iceland inazidi kuwa kutoka kwa barafu inayopungua

Mwaka 2014-2016

Afya

Desemba mwaka 2013 ukifunga pazia katika kijiji cha Meliandou nchini Guinea, mtoto Emile Ouamouno alifariki. Hii ilikuwa ni pigo kubwa kwa familia yake lakini kifo hicho kilikuwa na athari zaidi baada ya Emile kutajwa kama mgonjwa wa mwanzo kabisa wa ,mlipuko mbaya zaidi wa Ebola kuwahi kushuhudiwa.

Ugonjwa huo ambao huambukiza kwa haraka ulisambaa Guinea pamoja na nchi jirani za Liberia na Sierra Leone, na kujulikana kama mlipuko wa ebola magharibi mwa Afrika huku uchumi wa nchi hizo tatu na sekta za afya zikiathirika vibaya. Watu 6,000 walipoteza Maisha, jamii zikidhoofishwa na hofu kutanda.

 

Watafiti nchini Sierra Leone wakichunguza virusi vya Ebola kwa popo
Laura Gil / IAEA
Watafiti nchini Sierra Leone wakichunguza virusi vya Ebola kwa popo

Kufikia Agosti 2014 shirika la afya ulimwenguni, WHO lilitangaza mlipuko huo kuwa dharura ya afya ya umma kwa jamii ya kimataifa kwa ajili ya kuhakikisha msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa na kuzuia maambukizi katika nchi zingine.

Margaret Chan alikuwa mkurugenzi mkuu wa WHO wakati huo

Kwenye Mkutano wa 70 wa Afya Ulimwenguni mjini Geneva, Margaret Chan afanya muonekano wake wa mwisho kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Photo: WHO
Kwenye Mkutano wa 70 wa Afya Ulimwenguni mjini Geneva, Margaret Chan afanya muonekano wake wa mwisho kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

 

(Sauti ya Margaret)

“Hili ni janga la kijamii, janga la kibinadamu, janga la kiuchumi na tishio kwa usalama wa kimataifa nje zaidi ya maeneo ya mlipuko”

Ilichukua muda wa miaka miwili kwa WHO kutangaza kukoma kwa dharura hiyo ambapo kufikia wakati huo visa 28,616 vya ebola vilikuwa vimerekodiwa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leon na vifo 11,310.

Kwa bahati mbaya tangu mwaka 2018 sehemu nyingine ya Afrika imekuwa ikikabiliana na mlipuko wa pili kwa ukubwa wa ebola ambapo zaidi ya watu 2,200 wamepoteza maisha na watu 3,300 wameambukizwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mapigano kati ya makundi mawili yaliyogawanya kwa misingi ya dini ikiwemo waislamu na wakristo yaliwaacha watu na hofu kubwa huku ghasia zikisababisha wengi kufungasha virago na  kukimbia makwao.

Mwaka 2015, Umoja wa Mataifa uliadhimisha miaka 70 tangu kuasisiwa kwake, mwaka huo mwezi Septemba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa pamoja walipitisha Agenda 2030 ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ikiwemo lengo la elimu kwa wote, utawala bora,  nishati endelevu kwa wote, kwa lengo la kutokomeza umasikini katika mifumo yake yote.

Viongozi wa dunia mwaka huu wa 2015 wakapitisha pia mkataba wa makubaliano wa Paris kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi ambapo kwa mara ya kwanza nchi za ulimwengu waliahidi kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi na athari zake.

 Katibu Mkuu Ban Ki-moon, Christiana Figueres wa UNFCCC, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Rais wa COP21 wakisherehekea kihistoria kupitishwa kwa Mkataba wa Paris
Photo/UNFCCC
Katibu Mkuu Ban Ki-moon, Christiana Figueres wa UNFCCC, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Rais wa COP21 wakisherehekea kihistoria kupitishwa kwa Mkataba wa Paris

 

Uhasama wa kundi la kigaidi la ISIL sio tu ulisababisha watu kukimbia mashariki ya kati lakini kuzuka kwa vikundi matawi kote ulimwenguni vilizusha  hofu kubwa, nchini Kenya wanafunzi 147 walipoteza Maisha katika Chuo Kikuu cha Garissa, ndege ya Urusi ilishambuliwa na watu takriban 40 waliuwawa Beirut katika eneo la madukani na Paris Ufaransa zaidi ya watu 100 walipote Maisha baada ya kufiatuliwa risasi na wauaji  wa kujitoa mhanga

Mwaka wa 2015 rais wa Sudan Kusini Riek Machar alitia saini makubaliano ya amani kusitisha mzozo uliozuka mwaka 2013.

Uchaguzi wa rais ulifanyika Julai 2015 huku kukitajwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na zaidi ya wakimbizi laki moja wakikimbilia nchi jirani za Tanzania na Rwanda.

Mwaka 2016 kulishuhudiwa kuzinduliwa rasmi kwa Agenda 2030 kuendeleza pale malengo ya milenia yalifikia ukomo.

Mwaka huu pia wakimbizi walishiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya olimpiki, mwaka ambao ulishuhudia idadi ya wakimbizi kote duniani ikiongezeka na kufikia milioni 65,000.

Nchini Nigeria ukame na athari za kundi la Boko Haram mwaka 2016 vilisababisha ukosefu wa chakula na kusababisha Ofisi ya misaada ya dharura kuzindua ombi kubwa la dola bilioni moja.

Raia wa  Nigeria waliokimbia Cameroon kutokana na machafuko ya Boko Haram
UN Photo/Eskinder Debebe)
Raia wa Nigeria waliokimbia Cameroon kutokana na machafuko ya Boko Haram

 

Nchini Myanmar vikosi vya jeshi vilitajwa kutekeleza vitendo vya ukatili dhidi ya jamii ya warohingya.

Haiti yapata pigo tena kufuatia kimbunga Mathew ambako watu 600 walipoteza masha yao na nchi ikiachwa ikiwa imesambaratika sanjari na mlipuko mbaya wa kipindupindu ukishuhudiwa.

Mwaka 2016 Umoja wa Mataifa ulifanya kumbukizi ya aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros Ghali, na kumuaga Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliyehudumu kwa kipindi cha miaka kumi na kuteuliwa Katibu Mkuu mpya, Antonio Guterres.