WHO Afrika ilivyoisaidia Sierra Leone kuwa kinara wa kugundua magonjwa ya mlipuko
Kati ya mwaka 2014 mpaka 2016 kulitokea mlipuko wa ugonjwa mbaya zaidi wa Ebola katika nchi ya Sierra Leone na nchi jirani, mlipuko uliogharimu maisha ya zaidi ya wanawake, wanaume na watoto 4000 katika nchi hiyo. Wizara ya Afya ya nchi hiyo inaeleza kuwa tukio hilo la mlipuko wa Ebola lilikuwa la kushtukiza kwani walikuwa wana mfumo wa kawaida wa ufuatiliaji kwa kutumia karatasi au ujumbe mfupi kwa njia ya simu hali iliyofanya kupata taarifa kwa wakati kuwa chini ya asilimia 40.