Mabadiliko ya tabianchi

Vijana Kenya wavumbua apu ya simu itakayosaidia katika upandaji miti

Miti huchangia kwa kiwango kikubwa katika kutunza mazingira kwa kuzuia kuenea majangwa kupitia kuleta mvua na pia kutunza vyanzo vya maji ardhini. Kwa upande wa uchumi hali kadhalika, miti ina manufaa kama vile mbao.

Sauti -
3'46"

Wakati ni sasa kuchukua hatua kukomesha uchafuzi wa hewa:Guterres

Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu, ni wakati wakubadili hilo sasa Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua 

Sauti -
2'27"

07 SEPTEMBA 2020

Katika Jarida la Habnari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katika maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya rangi ya blu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka mshikamano kutokomeza uchafuzi wa hewa

Sauti -
12'51"

Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu, ni wakati wa kubadili hilo sasa:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya hewa chafu inayovutwa na watu 9 kati ya 10 kila uchao duniani kote.

Ziwa Turkana hatarini kukauka, uhai wa wanaolitegemea mashakani 

Nchini Kenya, ziwa Turkana ambalo ni ziwa kubwa la kudumu lililoko jangwani liko hatarini kukauka na hivyo kutishia uhai wa watu zaidi ya 300,000 wanaotegemea kipato chao kutokana na maji yake.

Hali ya hewa ya Morogoro haikuwa hivi, hatua za pamoja na za haraka zinahitajika-Wakazi wa Morogogo

Mkoa wa Morogogoro ulioko katika eneo la mashariki la Tanzania ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka mingi yametambulika kuwa maeneo yenye hali nzuri ya hewa kutokana na mazingira yake kuwa yenye misitu, nyika, na milima yenye kutiririsha maji safi.

Sauti -
3'36"

05 Agosti 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
-Lebanon,iko katika siku ya maombolezo kufuatia mlipuko mkubwa wa jana katika mji mkuu Beirut UNIFIL iko tayari kusaidia.
Sauti -
11'52"

Moto na kuyeyuka kwa barafu Arctic vyahitaji hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:WMO 

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO leo limesema joto kali la kupindukia na la muda mrefu Siberia limesababisha sehemu ya Arctic kuwa na joto kuliko kawaida na kuchochea kuzuka kwa moto wa nyika kwa mwaka wa pili mfululizo huku likionya pia kuhusu kupungua kwa kasi kwa barafu baharini kwenye pwani ya Urusi. 

COVID-19 imeongeza chumvi katika kidonda changu cha athari za mabadiliko ya tabianchi-Jemima Hosea 

Kutokana na mwamko wa watu nchini Tanzania kuyapenda mazingira ya nyumba zao, Jemima Hosea wa jijini Dar es Salaam, aliona hiyo ni fursa ya yeye kujipatia kipato kwa kuotesha na kuuza maua ya aina mbalimbali.

Sauti -
2'49"

Uhusiano kati ya biashara yetu na mazingira ni wa ajabu sana-Wauza miche ya miti Tanzania

Biashara ya uuzaji wa miche ya miti nchini Tanzania hususani katika jiji la Dar es Salaam ni ya miaka mingi. Wauzaji wanasema ingawa uhusiano kati ya miti na mazingira ni  wa wazi mno, lakini kwao uhusiano huu ni wa ajabu.

Sauti -
3'30"