Hala hala mlipuko wa homa ya Kongo na bonde wazuka Uganda: WHO

24 Januari 2018

Shirika la afya duniani WHO limeipongeza serikali ya Uganda kwa hatua za haraka kuweza kutambua mapema  kutokea kwa mlipuko wa homa iliyopatiwa jina la Kongo inayoenezwa na kupe aliyebeba virusi hivyo pamoja na homa ya bonde la ufa. Maelezo kamili anayo Siraj Kalyango.

Shirika la afya duniani WHO limeipongeza serikali ya Uganda kwa hatua za haraka kuweza kutambua mapema  kutokea kwa mlipuko wa homa iliyopatiwa jina la Kongo inayoenezwa na kupe aliyebeba virusi hivyo pamoja na homa ya bonde la ufa. Maelezo kamili anayo Siraj Kalyango.

(TAARIFA YA SIRAJ KALYANGO)

Pongezi hizo zimetolewa na mjumbe wa WHO Uganda Dkt Yonas Tegegn Woldemariam, katika taarifa kwa wandishi habari baada ya wizara ya afya kuthibitisha kuzuka kwa mlipuko wa homa hizo nchini humo.

Wizara ya afya imesema  maeneo yaliyoathirika kwa sasa ni wilaya za Nakaseke na Luwero umbali wa kilomita takriban 72 kaskazini mwa mji mkuu Kampala.

Taasisi ya utafiti wa virusi ya Uganda(UVRI) ilithibitisha vidudu vya homa ya kongo katika wilaya ya Nakaseke na hapo januari 18 2018, katika

Watu watatu kati ya saba waliokuwa wanashukiwa walikuwa jamaa wa karibu wa mgonjwa mmoja wa homa hiyo. Hata hivyo  matokeo ya sampuli kutoka kwa watu saba waliokuwa wanashukiwa hayakuonyesha dalili yoyote ya homa hiyo.

Kuhusu homa ya bonde la ufa , watu wanne wamehakikishwa kufariki kutokana na mlipuko huo kati ya wagonjwa wote watano na hii ikiwa mara ya pili homa  ya bonde la ufa kutokea nchini Uganda.

Akihutubia waandishi habari mjini Kampala waziri wa afya Dkr Jane Ruth Aceng amesema kuwa serikali imetumia mbinu zake za haraka kuweza kuingilia kati  kudhibiti milipuko hiyo, na kuwaomba wananchi wasiwe na hofu kwani hali imedhibitiwa.Waziri  pia ametoa tahadhari kwa  wanaoshughulikia nyama iliopikwa na maziwa moto kutumia vifaa vya kinga huku akifafanua kuwa nyama iliopikwa bbarabbara pamoja na maziwa yaliyochemshwa vizuri havisambazi magonjwa hayo.

Katika taarifa yake mjumbe wa WHO nchini humo ameitaja Uganda kama taifa lililo na mfumo bora wa uchunguzi ambao uliweza kugundua mapema na kuwajibika vilivyo na kuahidi kuwa shirika lake litaendelea kuiunga mkono serikali katika vita vya kudhibiti magonjwa hayo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud