Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yachukua hatua kudhibiti homa ya bonde la ufa

Nyama ambayo haijapikwa vizuri yawezasababisha kuenea kwa virusi mbalimbali vinavyosababisha magonjwa kwa binadamu. (Picha:UN /JC McIlwaine)

Uganda yachukua hatua kudhibiti homa ya bonde la ufa

Afya

Serikali ya Uganda imeanza kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mlipuko wa homa ya bonde la ufa pamoja na ile ya homa ya Kongo.

Serikali ya Uganda imeanza kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mlipuko wa homa ya bonde la ufa pamoja na ile ya homa ya Kongo.

Wizara ya afya inasema hadi sasa ni watu wanne ndio wanajulikana kufariki kutokana na mlipuko huo uliotokea katika wilaya za Luwero na Nakaseke  kilomita 70 na ushei kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala.

Waziri kutoka wizara ya afya anaehusika na masuala ya jumla  Sarah Opendi ameiambia Radio ya UN kuwa kuna mpango wa kuua kupe wakitumia dawa  mpya ya kunyunyuzia mifugo katika maeneo hayo.

OPENDI CUT1

Waziri afafanua jinsi  homa hizo jinsi zinavyoambukiza akieleza kuwa chanzo ni mdudu aina ya kupe.

OPENDI CUT2.

Muwakilishi wa shirika la afya dunini WHO nchini humo, Dr Yonas Tegegn kupitia taarifa amesema kuwa Uganda kama taifa lililotia sahihi kanuni za kimataifa za afya imefuata vilivyo masharti ya kutoa  taarifa  kuhusu visa vya homa ya bonde la ufa pamoja na ile ilipewa jina la homa ya kongo.