Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dondakoo wasalia “mwiba” Yemen- WHO

Wakimbizi wa ndani Yemen. Picha: OCHA

Dondakoo wasalia “mwiba” Yemen- WHO

Ugonjwa wa dondakoo unazidi kuwa tishio nchini Yemen baada ya kubainika kuwa hadi sasa hakuna chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea pamoja na vijana.

Shirika la afya duniani WHO linasema ingawa dozi 100,000 za kutibu dondakoo ziliwasili Jumatatu, dawa hizo ni kwa watoto walio na chini ya umri wa miaka mitano.

WHO imetaka hatua zaidi za kufungua mipaka ili misaada ya kibinadamu pamoja na dawa ziwafikie walengwa haraka ikwezekanavyo.

Hadi jana watu 197 walikuwa wameripotiwa kuugua dondakoo ambapo 22 kati yao wamefariki dunia.

Kando ya dondakoo ni ugonjwa wa kipindupindu ambapo visa zaidi ya  laki 9 na zaidi ya watu elfu 22 wamefariki dunia.