Shirika la afya duniani WHO, shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC, Madaktari wasio na mipaka MSF na shirika la Save the Children wanaisaidia serikali ya Msumbiji kupitia Wizara ya afya ya Msumbiji wameanza leo kusambaza chanjo ya matone ili kudhibiti kipundupindu na kuwalinda manusura wa kimbunga Idai mjini Beira nchini Msumbiji.