Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa washawishi wa mzozo Syria kuweka kando tofauti zao:Guterres

Ni wakati wa washawishi wa mzozo Syria kuweka kando tofauti zao:Guterres

Wakati mazungumzo ya amani ya Syria yameanza tena Geneva naziomba pande zote katika mzozo na hususani nchi zenye ushawishi kuelewa kwamba ni lazima kuleta amani Syria. Amina Hassan na taarifa kamili

(TAARIFA YA AMINA)

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António  Guterres alipozuru kambi ya wakimbizi ya Zaatari nchini Jordan mapema Jumanne.

Guterres ameongeza kuwa ni lazima pande hizo zielewe kwamba mzozo huo umekuwa tisho kubwa la utulivu sio kwa Syria pekee bali kwa kanda nzima na usalama wa kimataifa, kwani ugaidi umekuwa ukifaidika na mgogoro wa Syria na mingine duniani kote na kwamba

(SAUTI YA GUTERRES)

"Huu ni wakati kwa nchi zote zinazohusika moja kwa moja au kwa njia nyingine katika mzozo, kuweka tofauti zao kando na kuelewa kwamba , sasa kuna lengo la pamoja na lengo hilo la pamoja linatokana na ukweli kwamba wote wanatishiwa na hatari mpya ya ugaidi wa kimataifa.”

Ameongeza kuwa mamilioni ya wakimbizi wa vita vya Syria hawapati msaada wa kutosha na pia nchi zinazowahifadhi hiyo huu ni wakati wa kusema

(SAUTI YA GUTERRES)

"Endapo dunia itashindwa kuwasaidia wakimbizi , basi itakuwa inawasadia watu kama Daesh na al qaeida ambao wanatumia fursa hii kukusanya watu zaidi ili kuuweka usalama wa dunia hatarini. Mshikamano na wakimbizi wa Syria pia ni njia ya kuelezea uwezo wetu wa kuhakikisha usalama wa kimataifa"

Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria lakini pia kwa nchi zinazowahifadhi kama Jordan , Lebanon na nyinginezo.