Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia ni lazima ishikamane na kuwa na ujasiri 2018:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António-Guterres akihutubia baraza kuu kuhusu vipaumbele vyake kwa mwaka 2018. Picha na UN/ Eskinder Debebe.

Dunia ni lazima ishikamane na kuwa na ujasiri 2018:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameyataka mataifa duniani kuwa na kile alichoita umoja na ujasiri katika vita vya dhidi ya mgogoro unaondelea pamoja alichokiita hatari mpya. Katibu Mkuu António Guterres ametoa wito huo wa busara mjini New York Marekani hii leo wakati akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa, na kufafanua maeneo ambayo atayapa kipaumbele kwa mwaka huu wa 2018.

Katika ujumbe wake ametaja masuala 12 ya kuyatilia mkazo na kisha kusisitiza moja kubwa la kuwawezesha wanawake popote pale.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES-KATIBU MKUU)

“Kimsingi, dunia inarudi nyuma. Migogoro inazidi kupanuka na huku hatari mpya zikijitokeza. Na dukuduku la kupata silaha za kinukila limeongezeka duniani tangu vita baridi. Tabia nchi inakwenda kwa mwendo wa kasi sana kutuzidi .Pengo la kutokuwa na usawa nalo linapanuka. Tunashuhudia ongezeko la visa vya kutisha vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Utaifa,ubaguzi wa rangi pamoja visa vya chuki dhidi ya wageni vinaongezeka. Kwangu mimi naona hii ni ishara ya kuhitaji umoja zaidi pamoja na ujasiri ili kuweza kukabiliana vilivyo dhidi ya mtihani wa sasa kwa haraka, kupunguza hofu ya watu tunaowahudumia na kuipa dunia dira ya kufuata kuweza kupata mustakbali bora’’

Bwana Guterres ameongeza kuwa mataifa wanachama yanahitaji kuwa mstari wa mbele ingawa kila mmoja ,popote pale anaweza kufanya jambo ambalo linaweza kuufanya ulimwengu kuwa mahala bora zaidi kwa pamoja na salama.