Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanariadha wa kike wadhihirisha kuwa “sote tunaweza”

Wanariadha wa kike wadhihirisha kuwa “sote tunaweza”

Kushuhudia wanariadha wa kike wakishindana na kushinda kwenye michuano ya Olympiki ya mwaka huu, huko Rio de Janeiro, Brazili, inadhihirisha dunia kuwa sote tumeumbwa sawa na twaweza kufaulu.

Hiyo ni kwa mujibu wa Bi Beatrice Frey, meneja wa mitandao wa kijamii wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women ambaye amerejea kutoka Rio de Janeiro, Brazil wiki hii.

Bi. Frey amekuwa akishirikiana na kamati ya kimataifa ya olimpiki, IOC katika miradi tofauti ya kuwawezesha wasichana wadogo kujimudu zaidi kupitia kwa njia za michezo.

Michezo ya Olympiki ya mwaka huu imekuwa na idadi kubwa zaidi ya wanariadha wanawake ambapo asilimia yao ni 45.

Bi Frey anaelezea jinsi alivyojisikia kwa kushuhudia hali hiyo aliyoita ni maajabu.

(Sauti ya Beatrice Frey)

“Bila shaka Ibtihaj Muhammad mmarekani wa kwanza muislamu kushindana katika michezo za olimpiki akiwa amevalia hijab. Amesema kuwa anajivunia kuwahamasisha watu yeye akiwa mwanamke na mmarekani mweusi lakini amesema haipaswi kuwa hoja kubwa na anatumai siku moja vitu kama hivyo havitakuwa hoja kabisa.”