Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa mauaji dhidi ya raia Beni DRC ufanywe haraka: OHCHR

Uchunguzi wa mauaji dhidi ya raia Beni DRC ufanywe haraka: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kufanya haraka uchunguzi wa mauaji yaliyotokea Jumamosi Beni jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Watu 47, raia wakiwemo watoto wawili waliuawa na kundi la waasi la ADF, watu wengine wanne walijeruhiwa na nyumba 10 kuchomwa moto.
Mauaji hayo yanafanya idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na shinikizo la kundi la ADF tangu Januari 2014 kufikia watu 645,huku Umoja wa mataifa ukioredhesha vifo 237 vya raia. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu..
(SAUTI YA RAVINA)
"Tunaitaka serikali ya DRC kuongeza juhudi za kuwalinda raia, kuchunguza ukiukwaji huu mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kuhakikisha kwamba wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka pande zote wanafikishwa kwenye mkono wa sheria."