Mapigano Sudan Kusini yawafungisha virago maelfu zaidi na kuingia Uganda:

26 Julai 2016

Mapigano yalizuka mapema mwezi huu nchini Sudan Kusini hadi sasa yamewalazimisha watu 37,890 kukimbia nchini Uganda.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema, watu 70,000 sasa wanapata hifadhi Uganda na katika wiki tatu zilizopita , kumekuwa na wakimbizi wengi wanaowasili Uganda kuliko kipindi chote cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Adrian Edwards msemaji wa UNHCR hali bado ni tete ingawa mapigano yamepungua..

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

“Watu wapya wanaowasili wanaripoti kuendelea kwa mapigano, uporaji unaofanywa na wanamgambo wenye silaha, kuchomwa moto nyumba na mauaji ya raia.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter