Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na mauaji ya askari walinda amani Sudan Kusini

Ban asikitishwa na mauaji ya askari walinda amani Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon aamelaani vikali shambulio katika kituo cha ujumbe wa Umoja wa Matifa nchini Sudani Kusini UNMISS eneo liitwalo Akobo na kusababaisha vifo vya walinda amani wawili raia wa India huku mlinda amani mwingine akipelekwa katika kituo cha matibabu cha UNMISS.

Katika shambuliohiloraia kadaa ambao ni wakimbizi waliuwawa ambapo katibu mkuu Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za walinda amani waliopoteza maisha na serikali yaIndia.  Ban pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia za raia waSudanwaliouwawa katika shambulio la jana.

Katibu mkuu amezitaka pande zinazopigana kujizuia na kukomesha chuki. Ametaka chama tawala cha SPLM kudhihirisha maelewano na uongozi kwa niaba ya watu wa Sudan Kusini na kutatua tofauti zao kwa njia ya majadiliano haraka.