Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvumbuzi wa kimataifa na ushirikiano wa kikanda muhimu kwa ajira ya vijana:ILO

Uvumbuzi wa kimataifa na ushirikiano wa kikanda muhimu kwa ajira ya vijana:ILO

Mamilioni ya vijana duniani wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kupata ajira zenye hadhi, huku wengi katika sekta zisizorasmi wakighubikwa na umasikini na matumaini kidogo sana ya maisha yao ya baadaye. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani Guy Ryder akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa 105 wa kimataifa kuhusu masuala ya ajira.

Bwana Ryder amewaambia washiriki hao kwamba uwekezaji kwa vijana ni uwekezaji wa mustakhbali wa jamii nzima. Kwenye mkutano huo wajumbe wasikia mikakati na hatua za kuchukua ili kuwaingiza vijana wengi zaidi katika ulimwengu wa ajira , ikiwa ni pamoja na kujenga ushirika mzuri wa kitaifa na kimataifa ambao utachagiza ajira bora, kuwalenga vijana wa vijijini, na kutoa fursa ya kuboresha ujuzi wao wa kidijitali.