Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwongozo wa chakula unatoa fursa ya kuilinda dunia- FAO/Oxford

Mwongozo wa chakula unatoa fursa ya kuilinda dunia- FAO/Oxford

Shirika la chakula na kilimo FAO na chuo kikuu cha Oxford wametoa utafiti wa kimataifa juu ya mwongozo wa chakula kwa nchi zote duniani, kwa lengo la kuona endapo maamuzi ya nchi yana weka uhusiano kati ya mapendekezo ya chakula kwa ajili ya afya, na mazingira endelevu.

Utafiti huo mpya unatoa msukumo wa kushughulikia hali endelevu ya mabadiliko ya tabia nchi wakati wa kuchagiza lishe bora. Anna Islas Ramos ni afisa wa lishe kwenye shirika la FAO Roma anasema utafiti ulihusisha nne nne lakini nchi zote zinapaswa kuwa na mwongozo wa kitaifa..

(SAUTI YA ANNA)

Mwongozo wa lishe wa kitaifa una lengo la kuangalia watu wanakula nini kwa ajili ya lishe, hata hivyo ripoti inachopendekeza ni kutoa umuhimu kwa suala la mazingira wakati wanaweka mwongozo huo, kwa sababu chaguo lolote tunalofanya litakuwa na athari kwa mazingira."