Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Walinda Amani yaenzi ushujaa wa kapteni Diagne Rwanda

Siku ya Walinda Amani yaenzi ushujaa wa kapteni Diagne Rwanda

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa ya Walinda Amani ikishuhudia hafla maalum ya kuwaenzi walinda amani 129 kutoka nchi 50 waliopoteza maisha yao mwaka 2015 kutokana na mashambulizi, magonjwa au ajali. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats…

Tarumbeta zilizopigwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika wakati wa kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani tarehe 29 mwezi huu...

NAts ….

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake huu akasisitiza umuhimu wa jitihada za walinda amani katika kulinda raia, na kukuza maridhiano na amani.

Nats…

Baada ya tukio hili… kulifanyika hafla ya utoaji medali kwa mara ya kwanza kabisa ya ushujaa iitwayo medali ya Mbaye Diagne, kumuenzi Kapteni huyo aliyejitolea kuokoa makumi kadhaa ya wanyarwanda wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, njane wake Yacine Mar Diop akasema ..

(Sauti ya Bi Diop)

“ Kapteni Mbaye alikuwa ni mtu mzuri, mwenye bashasha, ukarimu, ambaye alikuwa anapenda kusaidia wenzake. Maisha yake yamekuwa mafupi sana lakini ameishi kama ameishi miaka mingi. Ametenda wema tu kabla ya kuondoka."