Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO:Kuna ongezeko kubwa la umri wa kuishi tangu 2000

WHO:Kuna ongezeko kubwa la umri wa kuishi tangu 2000

Umri wa kuishi kote duniani umeongezeka kwa kiasi kikubwa limesema shirika la afya duniani WHO Alhamisi, likitaja miaka mitano imeongezeka tangu mwaka 2000.

Kwa mujibu wa takwimu mpya za shirika hilo wanawake wa Japan na wanaume wa Uswis ndio wanaoishi muda mrefu zaidi kwa wastani wa miaka 86 na 81. Huku Sierra Leone ikitajwa kuwa wote wanaume na wanawake ndio wenye maisha mafupi saana ya miaka 50 tu.

WHO imeongeza kuwa ongezeko hilo la miaka 5 linatosha kubadili hali iliyoshuhudiwa katika miaka ya 1990 Afrika ya kupungua umri wa kuishi kutokana na ukimwi na kwa Ulaya Mashariki kutokana na kusambaratika kwa muungano wa Soviet.

Shirika hilo linasema mabadiliko makubwa ya kuishi yako Afrika ambako sasa watu wanatarajiwa kuishi kwa wastani wa miaka 9 zaidi sababu zikiwa kuimariska kwa afya ya watoto, kudhibiti malaria na ongezeko la fursa ya kupata dawa za kurefusha maisha kwa wanaoishi na HIV.

Hata hivyo wanawake bado wanawashinda wanaume kwa kuishi muda mrefu zaidi wastani ukiwa miaka mine na nusu zaidi baada ya kufikisha umri wa miaka 73.

Dr Ties Boerma, fwa WHO ametathimini takwimu za nchi 194...

(SAUTI YA DR BOERMA)

“Tofauti kati ya Ulaya na Afrika katika umri wa kuishi mwaka 2015 ni miaka 17, kwa Ulaya miaka 78 , wakati Afrika miaka 61. Na mwaka 200 0 ilikuwa miaka mitano zaidi”

Lakini sio habari njema kwa kila mtu, umri wa kuishi wa watoto wachanga katika nchi 22 za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara makadirio ya kuisni ni chini ya asilimia 60. Na bado kuna pengo katika upatikanaji wa huduma za afya.