Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mali kusimamia utekelezaji wa hukumu za MICT

Mali kusimamia utekelezaji wa hukumu za MICT

Umoja wa Mataifa na serikali ya Mali wamekamilisha makubaliano ya kusimamia utekelezaji wa hukumu zilizotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Rwanda, ICTR na mfumo uliochukua baadhi ya majukumu yake, MICT.

Katika makubaliano yaliyotiwa saini huko Bamako, Mali, Umoja wa Mataifa uliwakilishwa na msajili wa MICT John Hocking huku Jaji Sanogo Aminata Mallé, akiwakilisha Mali, nchi ambayo inashikilia magerezani mwake wafungwa 16 waliohukumiwa na ICTR.

Hatua ya hivi karibuni inaendeleza ile ya mwaka 2001 ambapo Mali ilikubali kutekeleza hukumu zinazotolewa na ICTR, ambapo Hocking amesema hatua ya Mali kuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba wa kutekeleza hukumu za MICT ni kithibitisho cha Mali kuunga mkono Umoja wa Mataifa na mfumo wa haki dhidi ya uhalifu.