Skip to main content

Njaa yahamisha raia Sudan Kusini

Njaa yahamisha raia Sudan Kusini

Shirika la la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbiai, UNHCR  linasema zaidi ya raia elfu 50 wa Sudan Kusini  wameamua kurudi Sudan. Wengi wao walirejea nyumbani Sudan Kusini baada ya taifa kuundwa wakiwa na matumaini ya kujenga upya maisha yao.

Hata hivyo machafuko nchini mwao Sudan Kusini yamesababisha njaa kwa mamilioni ya raia pamoja na madhila mengine ikiwamo magonjwa na kwa ujumla kuharibu mustakabali wa taifa hilo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo inayoonyesha misaada kwa wakimbizi hao.