Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahimiza Kenya kutofunga kambi za wakimbizi

UNHCR yahimiza Kenya kutofunga kambi za wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeeleza leo wasiwasi wake mkubwa, kuhusu uamuzi ulioripotiwa kutolewa na serikali ya Kenya ijumaa wiki iliyopita, wa kufunga kambi za wakimbizi nchini humo. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

UNHCR imeisihi serikali ya Kenya kuangazia upya uamuzi wake na kujizuia kuchukua hatua yoyote itakayoenda kinyume na wajibu wake wa kimataifa wa kuwapa hifadhi watu wanaokimbia hatari na mateso.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, imeripotiwa kuwa madhara ya kiuchumi, kiusalama na kimazingira yamesababisha uamuzi huo wa Kenya. Ikitambua mzigo mkubwa unaobebwa na Kenya, UNHCR imeipongeza pia nchi hiyo kwa kuchangia pakubwa katika kuwapa hifafhi mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini na Somalia kwa kipindi cha miaka ishirini na mitano iliyopita.

UNHCR imesisitiza kwamba, iwapo uamuzi huo utatekelezwa, wakimbizi wapatao 600,000 wataathirika.

Duke Mwancha ni Kaimu msemaji wa UNHCR nchini Kenya.

(Sauti ya bwana Mwancha)