Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wote lazima kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa Amani CAR:Ban

Wadau wote lazima kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa Amani CAR:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa wadau wote nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kuhakikisha uchaguzi wa Rais na wabunge unaofanyika leo unakuwa wa Amani na utulivu.

Ban ametiwa moyo na watu takriban milioni mbili waliojiandikisha kupiga kura hali ambayo amesema inaonyesha dhahiri ushiriki wa wananchi wa haki yao ya kidemokrasia.

Katibu Mkuu amerejelea kusema mpango wa Umoja wa mataifa nchini CAR MINUSCA unafanya kila liwezekanalo kwa ushirikiano na uongozi wa serikali kuhakikisha inazuia vitendo vyovyote vitakavyovuruga mchakato wa uchaguzi. Na amewataka wadau wote kushirikiana kwa karibu na MINUSCA kufanikisha hilo.