Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzinduzi rasmi wa SDG’s kuanza Januari Mosi: Ban

Uzinduzi rasmi wa SDG’s kuanza Januari Mosi: Ban

Siku ya mwaka mpya Januari Mosi inaashiria uzinduzi rasmi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 (SDG’s) iliyopitishwa na viongozi wa dunia Septemba mwaka jana kwenye Umoja wa Mataifa.

Ajenda hiyo mpya ya maendeleo inayataka mataifa kuanza juhudi za kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu SDG’s kwa kipindi cha miaka 15 ijayo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki-Moon malengo hayo 17 ni maono ya pamoja ya ubinadamu na mkataba wa kijamii baiana ya viongozi wa dunia na watu wao, ameongeza kuwa ni orodha ya mambo ya kufanya kwa watu na dunia na ni muongozo kwa ajili ya mafanikio.

Malengo hayo SDG’s yalipitishwa bila kupingwa na wanachama wote 193 wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa kihistoria hapo Septemba 2015, yakikijikita katika kushughulikia mahitaji ya watu katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea yakisistiza kwamba hakuna yeyote atakayeachwa nyumba.

Malengo hayo yaangalia mitazamo mitatu ya maendeleo endelebvu, kiuchumi, kijamii na kimazingira pamoja na vipengee muhimu vinavyoangalia masuala ya Amani, haki na taasisi muhimu.

Ban amesema kugeuza maono haya kuwa hali halisi ni jukumu la nchilakini litahitaji ushirikiano mpya na mshikamano wa kimataifa. Malengo hayo 17 yatakuwa yakifuatiliwa na kutathiminiwa kwa kutumia viashiria vya kimataifa.