Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya bora ya jamii na ustawi unahitaji uwekezaji:UNFPA

Afya bora ya jamii na ustawi unahitaji uwekezaji:UNFPA

Wakati nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGS wadau wa maendeleo yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajielekeza kutekeleza malengo hayo, mathalani lile la idadi ya watu UNFPA.

Katika ujumbe kupitia tovuti ya shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu Babatunde Osotimehin anasema lengo namba tatu ambalo ni afya bora na ustawi linahitaji serikali kuwekeza kwa kuhakikisha huduma za afya zinapatikana karibu na watu.

Kadhalika amesema vijana wanahitaji kupata huduma bora za afya na zaidi kufahamishwa kuhusu afya zao.

(SAUTI BABATUNDE)

‘‘Vijana wanahitaji kufahmau kuhusu miili yao, kwa kupata elimu ya kina ya utotoni na kupata huduma ili kuzuia mambo mengi. Kwa mfano, leo idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni miongoni mwa vigori kutoka Afrika. Kwa hiyo tukiwapa taarifa na teknolojia tunaweza kuwakinga na kufanya kazi nzuri.’’

Amesema utashi wa kisiasa, uongozi makini unahitajika pamoja na ushirikiano na asasi za kiraia na sekta binafsi katika kutimiza lengo hilo.