Mazungumzo ya Syria kuanza Geneva , kitovu cha majadiliano ya amani:

22 Disemba 2015

Majadialiano ya kujaribu kumaliza mgogoro wa Syria yataanza tena mjini Geneva Januari 2016 amesema leo Michael Møller, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa Geva alipozungumza na waandishi wa habari.

Bwana. Møller amesema nia ni mazungumzo kuanza mwishoni mwa Januari lakini kutatolewa taarifa Zaidi kuhusu mazungumzo hayo katika wiki za kwanza za Januari.

Amesisitiza umuhimu wa Geneva kama kitovu cha majadiliano ya Amani na suluhu ya migogoro.

(SAUTI YA Møller)

“Wakati dunia inaendelea kugawanyika Geneva inakuwa Zaidi na Zaidi chaguo kwa sababu ya sifa yake kama mahali ambapo unaweza kufanya masuala ya amani bila ajenda nyingine kuingilia na kwa sababu tuna miundombinu hapa ambayo imefanyiwa majaribiona imejengeka vizuri.

Akigusia kazi za mashirika ya Umoja wa Mataifa Geneva mwaka 2015 , Møller ameongelea tatizo la wahamiaji na wakimbizi Ulaya na kusema hilo ni moja ya mambo yanayopewa kipaumbe na ofisi ya Umoja wa mataifa Geneva katika kulitafutia ufumbuzi mwaka 2016.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter