Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa biashara ya kimataifa ubadilishwe : mtalaam wa UM

Mfumo wa biashara ya kimataifa ubadilishwe : mtalaam wa UM

Mtaalamu Huru kuhusu Uendelezaji wa Mfumo wa Biashara ya Kimataifa wenye Demokrasia na Usawa, Alfred de Zayas, amelaani shinikizo lililowekwa na nchi zilizoendelea dhidi ya nchi zinazoendelea kwenye mkutano wa mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani WTO uliofanyika mjini Nairobi nchini Kenya tarehe 15 hadi 19 Disemba mwaka 2015, akisema nchi hizo zimedhoofisha uendelezaji wa haki ya maendeleo.

Bwana de Zayas ameongeza kwamba ni lazima WTO iingizwe kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa na iheshimu kanuni za Mkataba wa Umoja huo.

Ameeleza kwamba kauli mbiu ya wakosoaji wa WTO ni dunia yetu haiuzwi, akisema ni dalili ya kuonyesha kwamba WTO inapaswa kubadilika sambamba na masharti ya maendeleo na haki za binadamu.

Hatimaye Bwana de Zayas amesisitiza kwamba lengo la biashara halipaswi kuwa manufaa ya makampuni makubwa, bali maendeleo ya binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa leo, makubaliano yaliyopatikana nchini Kenya, hasa yale yanayohusiana na habari na mawasiliano, yanapendelea kampuni za kibinafasi na nchi zilizoendelea.